HABARI

USIKOSE MIKUTANO YA GAiN TANZANIA

Usikose mikutano makini ya Gain Tanzania 2021 itakayofanyika katika ukumbi wa MORENA Hotel mji wa morogoro kuanzia tarehe 26 April hadi 01 May 2021

 

Ni Sehemu ya wewe kuonyesha ubunifu wako katika nyanja ya kitehama katika namna ya kupeleka utume mbele.

Utajifunza pia mbinu mbalimbali za kiteknolojia ambazo wengine hutumia kumwinua Kristo

Ni sehemu sahihi ya kujua mikakati mbalimbali ya idara ya mawasiliano ya kanisa la waadventista Tanzania inayotumia kuhakikisha injili inasonga mbele

 

KIINGILIO 50000

 

Wahusika

 

>Wakuu wa taasisi

>Makatibu Mhutasi wa ofisi za Konferensi na taasisi za kanisa

>Wachungaji wote wa mitaa

>Waratibu wa ACMS

>Makarani wa Kanisa

>Viongozi wa mawasiliano wa makanisa

>Wataalamu wa IT

>Waandishi wa habari

>Maofisa Mahusiano na wadau wengine wote wa mawasiliano

 

 

 

 

GAiN TANZANIA 2021

WIKI YA USHIRIKISHWAJI KWA VIJANA

Mpendwa msikilizaji wa Morning Star Radio na mtazamaji wa Hope Channel Tanzania, karibu kwenye juma lingine la ushirikishwaji kwa vijana (Total Youth Involvement). Juma hili litahitimishhwa jumamosi ya tarehe 30, Machi 2019.
Waweza kutushirikisha kinachojiri kanisani kwako katika ukurasa wetu wa facebook unaoitwa Morning Star Radio kwa kutumia hashtag #TYI19.

 

 

SHUKRANI KWA WALIOSHIRIKI KATIKA SIKU YA MATENDO YA HURUMA

Shukrani kwa wote walioshiriki kutoa damu katika siku ya matendo ya huruma (GYD 2019), iliyoongozwa na vijana na kufanyika tarehe 16/03/2019. Mungu awabariki

WIKI YA MATENDO YA HURUMA KWA VIJANA

Mpendwa mtazmaji wa Hope Channel Tanzania na msikilizaji wa Morning Star Radio katika juma hili tutabarikiwa na matendo ya huruma, yakiongozwa na VIJANA kutoka maeneo mbalimbali duniani ambalo kilele chake ni jumamosi ya Machi 16, 2019.

 

 

TAMC APP

Unaweza sasa  kufuatilia matangazo ya Hope Channel Tanzania na Morning star radio kupitia simu yako ya mkononi.

 Fungua playStore au appStore kisha download TAMC app sasa ufurahie na ubarikiwe .